Skip to main content

Neno la wiki- Ngekewa na Kismati

Neno la wiki- Ngekewa na Kismati

Katika neno la wiki  Januari 20, 2017 tunachambua maneno Ngekewa na Kismati, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Bakari anasema kwamba neno Ngekewa licha ya kawmba halitumiki sana kwenye Kiswahili na lina mshabaha na maneno kama vile bahati au kismati. Ngekewa ina maana kuwa na nyota nzuri, kwa mfano ukipanga jambo na liwe kama ulivyolipanga basi mtu huyu inasemekana umeangukiwa na ngekewa. Ngekewa ni tunu fulani, na maneno haya mawili yana maana sawa.