Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu Sudan Kusini awasili Juba

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu Sudan Kusini awasili Juba

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amewasili Juba nchini humo.

David Shearer raia wa New Zealand, ambaye atakuwa pia mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa Sudan Kusini UNMISS anachukua nafasi ya Ellen Margrethe Løj wa Denmark, aliyemaliza muda wake mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2016.

Baada ya kuwasili Juba Bwana Shearer alikuwa na haya ya kusema

(SAUTI YA SHEARER)

Nakuja na mtazamo safi na wazi kuhusu watu wa Sudan Kusini, ntatumia wiki zangu chache za mwanzo kusikiliza na kupokea yale watu watakayotaka kuniambia , nimejiandaa kwa kibarua hili, najua kutakuwa na changamoto, lakini nahisi watu wa Sudan Kusini wanastahili kuwa na taifa ambalo linalofanya kazi, linalowaangalia, lililo imara na linalowaletea amani na ustawi wao.”