Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu Burundi

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu Burundi

Umoja wa Mataifa nchini Burundi umezindua mpango wa mwitikio wa mahitaji ya kibinadamu ya dharura nchini Burundi, mpango unaolenga raia takribani milioni tatu ambao kutokana na majanga ya asili ikiwamo mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika mahojiano maaluma na idhaa hii, Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi , Abel Mbilinyi amesema mpango huo unaogharimu kiasi cha dola milioni 74 awali utawasaidia  watu milioni moja ambao wana uhitaji wa haraka.

Mbilinyi anaeleza umuhimu wa usaidizi wa haraka kwa wahitaji

( Sauti Mbilinyi)

Amesema cha upekee katika mpango huo ni.

( Sauti Mbilinyi)

Uzinduzi wa mkakati huo wa usaidizi wa kibinadamu umehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa serikali akiwamo Waziri wa Mambo ya nje wa Burundi, mwakilishi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na wahisani wakiwamo Marekani.