Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapitisha azimio kulaani jaribio la kuzuia demokrasia Gambia

Baraza la usalama lapitisha azimio kulaani jaribio la kuzuia demokrasia Gambia

(Natts….)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja mchana wa leo Alhamisi limepitisha azimio kulaani jaribio la Rais Yahya Jameh aliyeshindwa kwenye uchaguzi wa Desemba mwaka jana kukataa kuondoka madarakani.

Akifafanua kuhusu azimio hilo nambari 2337 la mwaka 2017, lililopitishwa bila kupingwa na wajumbe wote 15 wa baraza Rais wa baraza hilo balozi wa Sweden kwenye Umoja wa Mataifa Olof Skoog amesema

(SKOOG CUT 1)

“Azimio ambalo tumelipitisha linatoa idhinisho la kisiasa la baraza la usalama kwa ECOWAS na Muungano wa Afrika ili kuhakikisha kwamba matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa. Kuna ombi kwa Rais wa zamani Yahya Jameh kufanya utaratibu wa amani kukabidhi madaraka kwa Rais mteule ambaye sasa ameapishwa Adama Barrow. Matakwa ya watu wa Gambia na katika ya Gambia lazima viheshimiwe.”

image
Rais wa baraza la usalama balozi wa Sweden kwenye Umoja wa Mataifa Olof Skoog (kushoto). Picha: UN Photo/Eskinder Debebe
Kisha akaongeza

(SKOOG CUT 2)

“Azimio linasisitiza kwamba kila mtu ndani na nje ya Gambia ni lazima ajizuie na kuheshimu utawala wa sheria. Ni matumaini yetu sasa kwamba Rais wa zamani Jameh atakabidhi madaraka kwa amani kwa Rais aliyechakuliwa kidemokrasia muhala wake wa miaka mitano umekwisha”

Nao wajumbe wa baraza mmoja baada ya mwingine wakasisitiza umuhimu wa azimio hilo, Balozi Isobel Coleman mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu utawala na masuala ya kisiasa akasema

image
Balozi Isobel Coleman (kulia) mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu utawala na masuala ya kisiasa. Picha: UN Photo/Eskinder Debebe
(ISOBEL COLEMAN CUT)

“Watu wa Gambia wameweka Imani yao kwa ECOWAS na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha uhalali wa uchaguzi unalindwa hatupaswi kuwaangusha”

Naye balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Tekeda Alemu akisistiza umuhimu wa kuhakikisha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani na kurejelea mtazamo wa ECOWAS na Muungano wa Afrika ameonya

image
Balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Tekeda Alemu (kati). Picha: UN Photo/Evan Schneider
(SAUTI YA TEKEDA)

“Mtafaruku wa kisiasa nchini Gambia utakuwa na madhara makubwa sio tuu kwa nchi hiyo bali kwa ukanda mzima”

Rais mteule Adama Barrow ameapishwa leo rasmi katika nchi jirani ya Senegal. Baraza la usalama limesisitiza kuwa litaendelea kufuatilia hali nchini Gambia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atatoa ripoti kwa nchi wanachama hapo baadaye.