Maji taka yana tija kwa kilimo: FAO

Maji taka yana tija kwa kilimo: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO, linasema wakati umefika sasa maji taka yatumiwe katika kilimo na kutatua ukosefu wa rasilimali hiyo katika kilimo na ukosefu wa chakula.

Taarifa ya FAO inasema kuwa, maji taka yakitumiwa vyema yanaweza kusaidia moja kwa moja kukuza mazao kupitia umwagiliaji au kupitia uhifadhi wa maji katika ardhi ambao shirika hilo limeonya kuwa unapaswa kufanywa kwa tahadhari kubwa ya kiafya na njia sanifu.

Kwa mujibu wa FAO, matumizi ya maji taka katika nchi mablimbali ni miongoni mwa mada angaziwa katika mkutano wa siku tatu wa wataalamu ulioanza leo mjini Berlini Ujerumani .

Mkutano huo unaowaleta pamoja wadau wa kilimo,maji na mazingira, uatatumia mifano halisi ya miji ambamo umwagiliaji kupitia maji taka umefanuikiwa hasa kwa kuzingatia kuwa rasilimali hiyo hupatikana bure au kwa bei nafuu.