Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yachunguza mlipuko wa mafua ya ndege, Uganda

WHO yachunguza mlipuko wa mafua ya ndege, Uganda

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO lipo chonjo kukabiliana na mlipuko wa mafua ya ndege nchini Uganda, likiripoti kuwa lipo katika hatua za mwisho za kubaini anina ya virusi vilivyosababisha vifo vya ndege wengi katika wilaya za kati kati mwa nchi. John Kibego na maelezo zaidi.

(Taarifa ya John Kibego)

Benjamin Sensasi, Afisa wa Mawasilainao wa WHO, Uganda, amesema wakati huu ambapo hali haijawa ya kutiisha, wanaisaisdia serikali ya Uganda katika ufuatiliaji , uhamashishaji wa jamii na kufanya vipimo vya ngazi ya juu ili kubaini aina halisi ya virusi hivyo vya mafua ya ndege.

Asisitiza kuwa baado haijabainika iwapo virusi hivyo ni vile aina ya H7N9 kama ilivyoriporitwa katika ripoti ya wizara ya afya ya Uganda.

Ripoti ya WHO yatarajiwa kesho.

(Sauti ya Sensasi)

“Tutabaini siku ya Ijumaa. Bila shaka tunafahamu kwamba kuna mlipuko wa mafua ya ndege, kwa hiyo ufuatilaiji, na uhabarishaji wa umma na kuchukua vipimo katika mahabara vinaendelea”

Tayari Rwanda na Kenya zimepiga marufuku ya muda, uingizaji wa ndege na bidhaa zao kutoka Uganda ili kuzuia kusambaa kwa mafua ya cdege.