Ongezeko la ghasia za itikati kali magerezani ni changamoto:UNODC

Ongezeko la ghasia za itikati kali magerezani ni changamoto:UNODC

Ongezeko la ghasia zitokanazo na itikadi kali , kwa ujumla ni changamoto kubwa inayokabili uongozi wa magereza kote duniani kwa mujibu wa mwakilishi wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya dawa na uhalifu UNODC.

Vitisho vitokanavyo na watu kujihusisha na misimamo mikali vimekuwa vikiongezeka huku nchi zikijaribu kuongeza juhudi kukabiliana na itikadi hizo na ugaidi. Hivi karibuni kitengo cha masuala ya haki cha UNODC kimetoa muongozo mpya wa jinsi ya kudhibiti misimamo mikali miongoni mwa wafungwa na kuzuia ghasia. Philipp Meissner wa UNODC anaeleza ni kwa nini kudhibiti misimamo mikali magerezani ni jambo la kulipa kipaumbele.

(SAUTI YA MEISSNER)

“Linalotia hofu ni kwamba itikadi kali magerezani haijashughulikiwa ipasavyo, na kuleta changamoto kuu mbili, kwa upande mmoja uongozi wenyewe kuna idadi kubwa ya watu wanaoshikiliwa kwa madai ya ugaidi lakini pia udhibiti wa ghasia zitokanazo na itikadi kali ni mdogo miongoni mwa wafungwa na wanaweza kimsingi kushawishi wengi kuingia”