Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR,IOM wazindua mpango kukabiliana na janga la wakimbizi Ulaya

UNHCR,IOM wazindua mpango kukabiliana na janga la wakimbizi Ulaya

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR na la wahamiaji IOM pamoja na wadau 72 leo wamezindua mpango mpya kwa ajili ya kukabiliana na janga la wakimbizi na wahamiaji barani Ulaya 2017.

Mpango huo wa kikanda unalenga kuimarisha na kutilia mkazo juhudi za serikali za kuhakikisha uwezekano wa kuomba hifadhi na ulinzi wa wakimbizi na wahamiaji, aidha unalenga kusaidia katika kupata suluhu za muda mrefu kwa ajili ya usimamizi wa uhamiaji wenye utu.

UNHCR kupitia mkurugnezi wa ofisi ya Ulaya Vincent Cochetel umesema katika kipindi cha miaka miwili, mapokezi ya wahamiaji milioni 1.3 barani Ulaya yameghubikwa na changamoto nyingi ikiwemo sual ya ulinzi wa wakimbizi na wahamiaji hao na mpango huu unatoa muongozo katika kuhakikisha operesheni bora na mbinu bora za kukabiliana na hali hiyo mwaka 2017.

Naye msemaji wa IOM Leonard Doyle amesema wana wasiwasi mkubwa juu ya hatari na mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji watoto, wanawake na wasichana na mapngo huu ndio jawabu.