Ubelgiji yachanga euro milioni 14 kukabilia majanga na migogoro: FAO

Ubelgiji yachanga euro milioni 14 kukabilia majanga na migogoro: FAO

Serikali ya Ubelgiji , muungaji mkono mkubwa wa shughuli za dharura za shirika la chakula na kilimo FAO, imeongeza msaada wake katika kulinda kilimo kwenye nchi zilizokumbwa na mjanga.

Nchi hiyo imetoa Euro milioni 14 ambazo FAO inasema zitasaidia uwezo wa shirika hilo na nchi wanachama kukabiliana mara moja na majanga na migogoro , lakini pia kuimarisha juhudi za muda mrefu za kuhimili majanga kwa wakulima na wafugaji.

Baadhi ya fedha hizo zitatumika kuwapa uwezo wakulima katika miradi ya muda mrefu ambayo ni muhimu kwa kuboresha kilimo na kuhakikisha mavuno mazuri.

FAO imeishukuru serikali ya ubelgiji kwa machango huo ambao imesema itawaruhusu wakulima na wafugaji kusalia katika maeneo yao hata baada ya majanga.