Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP: Kila mtu anawajibika kufanya kila awezalo kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi

UNEP: Kila mtu anawajibika kufanya kila awezalo kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Zaidi ya watu milioni 7 kote duniani wanakufa kabla ya wakati wao kwa sababu ya hewa chafuzi. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim akizungumza na waandishi wa habari mjini  Davos, Uswis  kwenye kongamano la kimataifa la uchumi. Ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mtu kufanya kila awezalo kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. 

(Sauti ya Solheim-cut 1)

Mfano mwingine ni kwamba uhifadhi na ulinzi wa misitu iletayo mvua ni muhimu kama ule wa Indonesia itasaidia kukabiliana na hewa chafuzi na kuwapa wakulima fursa ya kuhifadhi ardhi, hii ikiwa ni sera nzuri ya kukabiliana na changamoto zilizopo na kuweza kufikia malengo.

Bwana Solheim amesema kuna fedha za kutosha ulimwenguni kutekeleza sera hizi bora na kwamba...

(Sauti ya Solheim- cut 2)

Kuna karibu dola bilioni elfu ishirini ambazo zipo ulimwenguni na cha muhimu ni kuanzisha miradi bora ili wawekezaji waione na kuifadhili.

Lazima tufanye kazi na benki kubwa, benki za bima, wasanifu wa hisa na kusimamia masoko ya hisa ili fedha hizi zitumike kwa miradi tuliyodhamiria kwa upande wetu.