Skip to main content

Asili-mto-asili-msitu kuokoa mazingira nchini Kenya

Asili-mto-asili-msitu kuokoa mazingira nchini Kenya

Nchini Kenya, mtandao wa wanafunzi duniani kwa maendeleo endelevu, WSCSD-Kenya umeibuka na mradi wa kusaidia kuboresha mazingira kwa kulinda misitu na mito nchini humo. Taarifa kamili na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Kwa mujibu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP mradi huo uitwao Asili- mto-asili-msitu, unaongozwa na Nickson Otieno na lengo ni kusaka suluhu endelevu kwa changamoto za mazingira zilizosababishwa na binadamu na hivyo kufanikisha malengo endelevu, SDGs.

Kupitia mradi huo ulioanza hivi karibuni, wanafunzi wanahamasishwa na kuelimishwa kulinda vyanzo vya maji na misitu kwenye mazingira ya shule na vyuo vyao ili kuwepo na mazingira ya kiafya kwa mujibu wa Ibara ya 42 ya Katiba ya Kenya.

Tayari mradi umeanza kutekelezwa katika mto Nairobi, ambapo wanafunzi wanakagua vimelea vilivyopo na taarifa kutumwa kupitia apu ya simu na kutathminiwa na hatimaye kubaina aina ya uchafuzi na suluhu kupendekezwa.

Mradi huo utasambazwa nchi nzima pindi mafunzo ya wakufunzi yatakapokamilika.