Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuki dhidi ya Waislamu haina tija-Guterres

Chuki dhidi ya Waislamu haina tija-Guterres

Umoja wa Mataifa leo umezindua kampeni iitwayo Pamoja yenye lengo la kukabiliana na chuki na ubaguzi dhidi ya waislamu duniani. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Uzinduzi umefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja viongozi waandamizi wa chombo hicho, wawakilishi wa serikali na mashirika ya kiraia.

Katibu Mkuu António Guterres akatoa ujumbe wake kwa njia ya video akisema kuwa uwepo wa wahanga wa ukosefu wa stahamala na hofu havionekani kwenye takwimu bali hushusha utu wa mtu na ubinadamu, hivyo akasema.

( Sauti Guterres)

"Lazima tukatae jitihada za kejeli za kugawanya jamii na kuona jirani kama watu tofauti. Ubaguzi unatuteketeza sote. Unazuia watu na jamii kufikia uwezo wao waliojaliwa."

Guterres amesema ni muhimu kuimarisha ujumuishwaji na stahamala kwani.

( Sauti Guterres)

"Watu popote walipo wanahitaji kuhisi kuwa utambulisho wao wa kitamaduni unathaminiwa na wakati huo huo wajione wanakubalika katika jamii nzima."

Katibu Mkuu amesema uwepo wa mjumuiko wa utamudni ni jambo chanya hivyo .

( Sauti Guterres)

"Pamoja, hebu tujenga madaraja.Pamoja, hebu tubadili hofu iwe matumaini."