Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa mishahara kuengua vikosi vya Burundi AMISOM

Ukosefu wa mishahara kuengua vikosi vya Burundi AMISOM

Serikali ya Burundi imeanzisha utaratibu wa kisheria wa kuondoa vikosi vyake vya kulinda amani kwenye muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM. Hii ni baada ya Shirika la Muungano wa Ulaya ambao ni wafadhaili wa muungano wa Afrika (AU) kuzuia mishahara ya wanajeshi wa Burundi walioko katika vikosi vya AMISOM kwa miezi 12 sasa . AU imeutaka Muungano wa Ulaya kutoa malipo bila ubaguzi kwa wachangiaji wote wa vikosi vya AMISOM. Burundi ina jumla ya wanajeshi 54OOwanaolinda amani Somalia.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi

(TAARIFA YA KIBUGA)