Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni kuchagiza maendeleo endelevu yazinduliwa uwanja wa ndege wa Zurich

Kampeni kuchagiza maendeleo endelevu yazinduliwa uwanja wa ndege wa Zurich

Kampeni bunifu ya kuchagiza maendeleo endelevu imezinduliwa katika uwanja wa ndege wa Zurich nchini Uswis na itaendelea hadi  tarehe 22 Januari kama sehemu ya jitihada za kueneza habari kwa watu bilioni mbili kati ya sasa na mwaka 2030.

Kampeni hiyo kwa kutumia michezo ya video na mtandao kupitia  hashtag #YouNeedToKnow au unahitaji kufahamu, inawalenga wasafiri waweze kuona wakati wanapopita kwenye uwanja huo.

 Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa Bi Aziyade Poltier Mutal  wa Umoja wa Mataifa amesema…

 (Sauti ya Aziyade)

 Kampeni hii ya #YouNeedToKnow au unahitaji kufahamu  imezinduliwa baina yetu na maduka yanayouza bidhaa mbali mbali bila ushuru kwenye viwanja vya ndege,

nia yetu ni kuchagiza wasafiri takriban bilioni mbili kufikia mwisho wa mwaka 2017 kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu na leo tuanzisha kampeni hii hapa Zurich wakati wa kongamano la kimataifa la uchumi Davos.

Inakadiriwa kuwa wastani wa abiria milioni mbili hupita uwanja wa ndege wa Zurich  kila mwezi. Kampeni hii ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mjini Geneva mwezi Novemba mwaka jana na kusambazwa hadi Heathrow London mwezi Desemba.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wasafiri wanaowasili wapashwa habari kuhusu  SDGs na kuhamasishwa kutimiza jukumu lao kuhakikisha kufikia malengo hayo ifikapo mwaka 2030. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Michael Møller amesema kuwa hii ni nafasi mojawapo ya kuwakumbusha abiria kote duniani juu ya malengo hayo.