Skip to main content

Uonevu huathiri mtoto mmoja kati ya wanne shuleni-UNESCO

Uonevu huathiri mtoto mmoja kati ya wanne shuleni-UNESCO

Kukiwa na watoto zaidi ya bilioni moja shuleni kote duniani, takribani robo yao hukabiliwa na uonevu umesema Umoja wa Mataifa.

Takwimu hizo zinazotoa hofu zimetolewa Jumanne kwenye ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, ambayo inaainisha kwamba , walio katika hatari zaidi mara nyingii ni masikini au wanaotoka katika makabila, lugha au utamaduni wa walio wachache.

Aina mpya ya uonevu kama vile wa kutumia mtandao, pia unaathiri maisha ya watoto kama anavyofafanua Christopher Castle wa UNESCO.

(SAUTI YA CHRISTOPHER)

“Ni tatizo kubwa inakadiriwa karibu watoto milioni 246 na vijana kote duniani wanakabiliwa na ghasia uonevu shuleni kila siku. Hivi sasa nchi, sekta za elimu na shule zimezinduka na ukwewli kwamba hili ni tatizo lililopuuzwa kwa muda mrefu.”

Ameongeza kuwa sababu ya kushika bango hivi sasa ni kusisitiza kuwa ili watoto wawe na mazingira bora ya kusoma ukatili na uonevu mashuleni hauna nafasi na ni lazima ukomeshwe.