Skip to main content

Homa ya mafua ya ndege yazuka Uganda

Homa ya mafua ya ndege yazuka Uganda

Serikali ya Uganda imetangaza mlipuko wa mafua ya ndege aina ya H7N9, ambapo mizoga kadhaa ya ndege imekutwa katika wilaya za katikati mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Kutoka Uganda, hii hapa ripoti ya mwandishi wetu John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Kulingana na Waziri wa Kilimo, Viwanda na Uvuvi, Christopher Kibazanga, vipimo vilivyofanywa nchini humo vimethibitisha mlipuko wa mafua ya ndege yenye virusi vinavyosambaa upesi na kusababisha vifo vingi zaidi kwa binadamu na wanyama.

Amesema mnamo tarehe pili mwezi huu wa Januari, mamlaka wa wanyamapori waliripoti vifo vingi vya ndege.

Pia mnamo 13 mwezi huu, bata 16 wakufugwa waliripotiwa kwambukizwa virusi vya mafua ya ndege wilayani Masaka na visa vingine kadhaa kuripotiwa wilayani Kampala.

Wizara hiyo bado haijatoa takwimu kamili za ndege walioathirika na wala kiwango cha mambukizo ya virusi hivyo vya H7N9.