Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki wa kupindukia unaendelea Sudan Kusini:Ripoti

Ukiukwaji wa haki wa kupindukia unaendelea Sudan Kusini:Ripoti

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili vikiwemo mauaji , unbakaji na kukiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu umefanyika juba Sudan Kusini wakati na baada ya machafuko yaliyozuka kati ya Julai 8 na 12 mwaka 2016.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS na ofisi ya haki za binadamu iliyochapishwa Jumatatu ikisistiza kwamba miezi sita baada ya machafuko hayo kuna ukwepaji mkubwa . Eugene Nindorera mkurugenzi wa haki za binadamu wa UNMISS anasema hatua zimeanza kuchukuliwa

(SAUTI YA EUGENE)

“Tumeshuhudia baadhi ya hatua zikilichukuliwa, kwa kuwa serikali imeunda kamisheni maalum kuchunguza kile kilichotokea Terrain, na baadhi yao walikamatwa na tunatumai kuwa watafikishwa mbele ya mahakama maalum kwa mujibu wa kile ambacho serikali imedokeza.”