Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu husaidia hata jamii zenye migogoro: Hongbo

Takwimu husaidia hata jamii zenye migogoro: Hongbo

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu takwimu umeanza leo huko  Cape Town, Afrika Kusini ambapo imeelezwa kuwa dhana ya matumzi ya takwimu sahihi  yaweza kutumiwa kusaidia ustawi wa nchi zenye migogoro pia.

Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa Wu Hongbo ambaye amezungumza na Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wa takwimu sahihi na kutosha kwa kila taifa ili kufanikisha utaratibu wa maendeleo

Akitoa mfano kwa ajili ya umuhimu wa takwimu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa kila taifa amesema...

(Sauti ya Wu) 

Ukichukua mfano wa usajili wa vizazi na vifo katika taifa lolote bila ya kuwa na takwimu sahihi mpangilio wa kupanga miji, ajira au elimu haiwezi kufanikishwa. Kuna karibu nchi wanachama 100 ambazo hazina takwimu sahihi na uwezo wa kuzipata. Kwa hivyo kuna haja kufahamu changamoto zinazowakabili nchi zinazoendelea hasa katika suala hili na na kuhimiza ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea na zile za pato la chini, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.

Juu ya nchi zinazokabiliwa na migogoro, Wu amesema …..

(Sauti ya Wu)

Takwimu sawa na haki ni muhimu na kupatikana kwa wakati unaotakikana hata kwa nchi zilizo kwenye migogoro. Kwa mfano katika nchi hizi kama hawana takwimu za saw juu ya idadi ya wakimbizi kwenye kambi, watoa misaada hawawezi kujua namna ya kugawa chakula au kupeana misaada muhimu inayohitajika. Ukweli ni kwamba uhusiano kati ya amani na kutekeleza maendeleo, bila amani maendeleo hayawezi kufanyika, bila maendeleo, amani na usalamu endelevu havitaweza kupatikana.

Ametaja kuwa jukwaa hili litawapa fursa sio tu maafisa wa serikali bali pia wajasiriamali wote katika sekta binafsi ambapo takribani 1,500 wanatarajia kushiriki.