Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rumba ya Cuba ni turathi iliyotuzwa na UNESCO

Rumba ya Cuba ni turathi iliyotuzwa na UNESCO

Rumba ya Cuba inahusishwa na utamaduni wa Afrika lakini pia inachanganya na utamaduni wa hispania. Utamaduni  huu nchini Cuba umeshamiri zaidi kwenye vitongoji vya watu wa kipato cha chini na vijijini kuanzia magharibi hadi mashariki mwa nchi hiyo. Miondoko yake, mbwembwe na hisia zitokanazo na mtindo huu wa dansi ni dhihirisho la utamaduni ambao shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetambua na kuingiza kwenye orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Je rumba hii nini hasa? Amina Hassan anakupeleka Mantanzas, mashariki mwa Cuba kufahamu zaidi..