Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahakikisha matokeo ya uchaguzi Gambia yanaheshimiwa- Chambas

Tunahakikisha matokeo ya uchaguzi Gambia yanaheshimiwa- Chambas

Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo wamekutana ili kupokea taarifa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu huko Afrika Magharibi na kushauriana kuhusu ukanda huo, ambapo wameelezwa kuwa juhudi zinaendelea ili kuhakikisha Rais wa Gambia aliyeshindwa uchaguzi hivi karibuni anaachia madaraka. Assumpta Massoi na taarifa kamili

( TAARIFA YA ASSUMPTA)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya umoja huo ukanda wa Afrika Magharibi UNOWAS, Mohamed Ibn Chambas amelimbia baraza hilo kuwa UNOWAS inatambua na kuzingatia majadiliano yanaoongozwa na jumuiya ya kiuchumi Afrika Magharibu ECOWAS katika kuhakikisha Rais liyeshindwa Yahaya Jameh anaachia madaraka na hivyo kuruhusu Rais mteule Adam Barrow kuapishwa.

Amesema juhudi zinaendeea matahalani.

( Sauti Ibn Chambas)

‘‘Ujumbe wa ngazi ya juu wa ECOWAS umerejea mjini Banjul leo Januari 13 katika majaribio ya kumshawishi Rais Jameh kukubali matokeo na kuondoka madarakani.’’

Amesema ikiwa ushawishi utashindikana mkakati ni.

( Sauti Ibn Chambas)

‘‘Kutumia kila mbinu ikiwamo ymatumizi ya nguvu kuhakikisha matakwa ya watu wa Gambia yanatimizwa. Ikilazimu hivyo, ECOWAS inatarajia kusaka ridhaa ya baraza la usalama la Muungano wa Afrika na baraza hili ili kutuma vikosi Gambia.’’