Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi DAVOS teteeni haki za binadamu- Zeid

Viongozi DAVOS teteeni haki za binadamu- Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ametoa wito kwa viongozi watakaokutana huko Davos, Uswisi wiki ijayo kutumia ushawishi wao kutetea haki za binadamu na kuzuia vitendo hivyo kokote wanakojihusisha na biashara.

Katika taarifa yake, Zeid amesema wito wake unazingatia kuwa mwaka huu wa 2017 umeanza kukiwa na hofu kubwa juu ya ongezeko la sera za mgawanyiko, chuki na mashambulizi dhidi ya haki za binadamu na udhibiti wa rasilimali za kiuchumi kwa baadhi ya watu.

Amesema sheria na misingi ya tamko la haki za binadamu ambazo zilipiganiwa kwa dhati, sasa ziko hatarini hivyo viongozi wa kibiashara wanaokutana Davos wana dhima kuu ya kuondoa ongezeko hilo na badala yake wapigie chepuo haki za binadamu kule wanakoendesha biashara zao.

Mathalani ametaka kampuni zieleze bayana kuwa shughuli zao hazitakinzana na haki za binadamu huku akipongeza kampuni ambazo zimeanza kuchukua hatua ikiwemo benki kusitisha miradi ambayo inakiuka haki za bi