Bi. Patriota ateuliwa naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Colombia

Bi. Patriota ateuliwa naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Colombia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Tania Patriota wa Brazil kuwa naibu mwakilishi wake maalum nchini Colombia.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bi. Patriota ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 na Umoja wa Mataifa kwenye kazi ya kukuza maendeleo na kushughulikia majanga atakuwa naibu mkuu pia wa ujumbe wa umoja huo huko Colombia.

Kwa kipindi cha miaka 13 iliyopita alifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Brazil, Haiti, Colombia na Mongolia na vile vile katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akiwa mwakilishi mkazi wa UNFPA, Haiti alishiriki katika jitihada za usaidizi wa kibinadamu za wa Umoja wa Mataifa kufuatia tetemeko la ardhi la mwaka 2010.

Bi. Patriota ana utaalamu wa kina katika nyanja za afya ya umma, idadi ya watu, maendeleo na kukabili ukatili wa kijinsia.