Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cyprus yahitaji makubaliano endelevu na thabiti- Guterres

Cyprus yahitaji makubaliano endelevu na thabiti- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ametaka uvumilivu katika kusaka suluhu ya mzozo wa Cyprus inayolenga kuunganisha kisiwa hicho baada ya kuganywa mwaka 1974 kati ya wacyprus wenye asili ya Uturuki na wale wenye asili ya Ugiriki. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Guterres amesema hayo mjini Geneva, Uswisi hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushiriki mkutano wa pande mbili hizo, ukijumuisha kiongozi wa wenye asili ya Ugiriki Nicos Anastasiades [ANASTASIADES] na wa asili ya Uturuki Mustafa Akinci [AKINCHI]

Amesema hakuna miujiza na kinachotafutwa ni

(Sauti ya Guterres)

“Suluhu thabiti na endelevu kwa Jamhuri ya Cyprus na kwa jamii za Jamhuri ya Cyprus.”

Amesema makubaliano si ya viongozi kwani itabidi yapigiwe kura ya maoni na wananchi…

(Sauti ya Guterres)

“Kwa hiyo tuwe na suluhisho litakaloridhiwa kikamilifu na pande husika na likubaliwe kabisa na wananchi, la sivyo hatutaweza kufikia lengo.”

Katibu Mkuu amewapongeza Anastasiades na Akinci kwa jinsi walivyojitolea kwa miezi 20 sasa kusimamia mazungumzo hayo, akisema Umoja wa Mataifa kwa upande wake ni kuweka mazingira bora makubaliano yatakayofikiwa yaweze kutekelezwa.