Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wahitaji vifaa vya baridi Darfur: OCHA

Wakimbizi wahitaji vifaa vya baridi Darfur: OCHA

Wakimbizi wengi wa ndani jimboni Darfur, nchini Sudan wanahitaji misaada ya dharura ili kujikinga na baridi kali inayofikia hadi nyuzi joto saba au chini zaidi majira ya usiku huko Jebel Marra, imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Kwa mujibu wa OCHA, wakimbizi hao waliofurushwa makwao mwaka jana, wanahitaji vifaa kama vile mablanketi na nguo za kuhifadhi joto pamoja na mafuta kwa ajili kupikia na kuhifadhi joto wakati huu ambapo usalama umezorota na hivyo wanashindwa kusaka kuni nje ya kambi zao.

OCHA imesema kuwa mashirika kadhaa ya kiraia yanaendelea kufanya tathimini ya idadi kamili ya wakimbizi wa ndani wanaohitaji misaada ya malazi na mahitaji mengine ya majumbani.

Machafuko ya hivi karibuni huko Jebel Marra, yamesababisha wakimbizi wa ndani 80,000 mwaka jana mjini Darfur Kati.