Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamabolo ateuliwa kuongoza UNAMID

Mamabolo ateuliwa kuongoza UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU, Nkosazana Dlamini-Zuma, leo wametangaza uteuzi wa Jeremiah Nyamane Kingsley Mamabolo wa Afrika Kusini,kuwa Kaimu mwakilishi wa ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur Sudan, UNAMID.

Mteule huyo anachukua nafasi ya Martin Ihoeghian Uhomoibhi wa Nigeria, ambapo viongozi hao wamemshukukuru kwa utumishi wake.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu kuhusu uteuzi huo, imesema kuwa Mamabolo ana uzoefu katika kufuatilia masuala ya Darfur, pamoja na mambo ya kidiplomasia, kwani tangu mwaka 2016 amekuwa Naibu mwakilishi wa masuala ya siasa, haki za binadamu na sheria katika UNAMID.

Kiongozi huyo amewahi kushika nyadhifa tofauti za kidiplomasia ikiwamo ya kuwa mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2016.