Skip to main content

Uchumi wafufuliwa huku mgogoro ukitatuliwa Yemen: Cheikh

Uchumi wafufuliwa huku mgogoro ukitatuliwa Yemen: Cheikh

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, leo amekamilisha ziara yake mjini Riyadh ambapo amekutana na maafisa wa Yemen na Saudi na kuwaleza mchakato wa amani nchini Yemen ikiwamo hatua za usitishwaji wa mapigano.

Katika ziara yake pia amekutana na Gavana wa benki kuu ya Yemen na kujadili naye hali ya kiuchumi na hatua za dharura na muhimu katika kuepusha mdororo zaidi wa kiuchumi.

Amesema fedha mpya zilizochapishwa zimeanza kuwasili Yemen ikiwa ni sehemu ya kukwamua uchumi wa taifa hilo na kusisitiza kuwa serikali na wadau wengine wachukue hatua zitakazowezesha kuanza kwa malipo ya mishahara wakati huu ambapo ukata unatatuliwa.

Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa huko Yemen anatarajiwa kufanya ziara Doha, Muscat, Amman , Eden na Sana'a ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaka suluhu ya mgogoro nchimi humo.