Utafiti watia hofu kuhusu homa ya ini aina ya C Syria

Utafiti watia hofu kuhusu homa ya ini aina ya C Syria

Shirika la afya duniani, WHO limesema utafiti uliofanywa miongoni mwa watu zaidi ya 20,000 nchini Syria umebaini idadi ya kutia hofu ya watu wenye homa ya ini aina ya C, hasa wale walio hatarini zaidi kuambukizwa ugonjwa huo.

Mathalani asilimia 14.4 ya wagonjwa wa figo wanaopata tiba ya kuondoa sumu mwilini, walikutwa na maambukizi ya homa hiyo ya ini.

Hata hivyo mambukizi ya homa ya ini aina ya B yamepungua miongoni mwa vijana na watoto kutokana na kampeni ya kitaifa ya chanjo iliyoanzishwa mwaka 1993 nchini Syria ilhali kiwango kikubwa kikiwa ni miongoni mwa watu wazima.

Kufuatia matokeo ya utafiti huo, WHO na Wizara ya Afya wanaandaa mkakati madhubuti wa kudhibiti virusi ya homa ya ini wakiangazia zaidi mipango ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.