Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dhibiti tumbaku uongeze kipato- Dkt. Ouma

Dhibiti tumbaku uongeze kipato- Dkt. Ouma

Hii leo shirika la afya ulimwenguni, WHO limechapisha ripoti yenye kurasa zaidi ya 700 inayoweka bayana faida za kiuchumi za kudhibiti matumizi ya tumbaku na bidhaa zake. Ripoti hiyo inayotokana na utafiti uliofanywa kwa kina inaeleza kuwa hatua mbali mbali zinaweza kuchukuliwa kuhakikisha kuna sera thabiti ambazo kwazo tumbaku inadhibitiwa na hivyo hatimaye serikali inapata kipato, wananchi halikadhalika.

Je ni kwa vipi hili linaweza kuleta unafuu kwa mwananchi wa kawaida? Je kuna nchi ambazo zimefanikiwa kudhibiti tumbaku katika zama za sasa ambazo kampuni nazo za tumbaku zimesimama kidete kushawishi wakulima hata kwa kuhakikisha wanawalipa mapema pindi wanaponunua tumbaku tofauti na mazao mengine? Assumpta Massoi amezungumza na Dkt. Ahmed Ouma, mshauri wa masuala ya tumbaku ofisi ya WHO kanda ya Afrika ambaye anaanza kwa kuelezea ripoti inalenga nini.