Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokukubaliana kwa awali kusituzue kuchukua hatua sasa- Guterres

Kutokukubaliana kwa awali kusituzue kuchukua hatua sasa- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema lengo la msingi la kuanzishwa Baraza hilo la kuzuia vita liko mashakani, ikiwa ni zaidi ya miaka 70 tangu kuanzishwa chombo hicho. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

 Nats..

Rais wa Baraza la Usalama akiitisha kikao cha Baraza ajenda kuu ikiwa ni kuzuia mizozo na uendelezaji wa amani.

Katibu Mkuu António  Guterres ikiwa ni kikao chake cha kwanza akasema mamilioni ya watu wanaangalia chombo hicho kupata suluhu la mizozo inayowakabili, huku baraza likisalia na mgawanyiko..

(Sauti ya Guterres-1)

 “Fursa nyingi za kuzuia mizozo zimepotea kwa kuwa mwanachama haamini nia ya mwenzake na kwa sababu ya masuala ya mamlaka za kitaifa. Hofu hizo zinaeleweka kwenye dunia ya sasa yenye uthabiti tofauti na misingi inayotumiwa kitofauti.”

 Hivyo amesema..

“Kutokukubaliana siku za nyuma kusituzuie kuchukua hatua hii leo. Sote kwa pamoja tuonyeshe uongozi na tuimarishe uhalali na mamlaka ya Umoja wa Mataifa kwa kuweka amani mbele.”

Katibu Mkuu amesema kwa sasa muda mwingi sana na rasilimali nyingi vinatumika kushughulikia majanga badala ya kuyazuia. amesema watu wanalipa gharama kubwa, nchi wanachama halikadhalika, na hivyo ni lazima kuanzisha mfumo mpya kabisa, akipatia msisitizo mfumo wa kuzuia majanga badala ya kusubiri yatokee.