Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia waliozingirwa mjini Mosul Iraq, wanateseka: OCHA

Raia waliozingirwa mjini Mosul Iraq, wanateseka: OCHA

Wakimbizi wa ndani nchini Iraq hususani katika maeneo yanayokaliwa na vikosi vya kundi la kigaidi la ISIL wanakabiliwa na mateso makali wakati huu ambapo kikundi hicho kinaendelea kushikilia eneo la Magharibi mwa Allepo na hivyo kuzuia ufikishwaji wa misaada, umesema leo Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali nchini Iraq na juhudi za ukwamuaji wa raia, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Jens Larke, amesema manusura kutoka Maghraibi mwa Mosul wanasimulia mikasa ya kuogofya.

( Sauti livyo Jens Larke )

‘‘Kulingana na ripoti za kiusalama kuhusu eneo hilo, kuna bidhaa chache sana za mahitaji muhimu zilizosalia mthalani vyakula. Pia wanasema kwamba wanazuiwa hata kutumia mashine ya kuzalisha umeme yani genereta’’.

Zaidi ya watu 130,000 wamekombolewa kutoka katika maeneo yanayokaliwa na ISIL mashariki mwa Mosul.