Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio la kigaidi Misri.

Baraza la usalama lalaani shambulio la kigaidi Misri.

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali shambulio la kigaidi nchini Misri, waliloliita la uoga, lililotekelzwa hapo jana na kugharimu maisha ya askari tisa na kujeruhi wengine zaidi ya13.

Taarifa ya wajumbe wa baraza hilo imeeleza rambirambi za kina za baraza hilo kwa familia za wahanga na serikali ya Misri, na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi.

Ugaidi katika aina zake zote na udhihirisho wake, unachochea moja ya tishio kubwa katika amani na usalama wa kimataifa imesema taarifa hiyo.

Baraza limesisitiza pia umuhimu wa kuwafikisha watekelezaji, waandaji, wawezeshaji na wadhamini wa kitendo hicho cha kigaidi katika mkono wa sheria.