Katibu Mkuu alaani mashambulizi ya kigaidi huko Yerusalemu

Katibu Mkuu alaani mashambulizi ya kigaidi huko Yerusalemu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa na mpalestina mmoja huko Yerusalemu siku ya Jumapili.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Bwana Guterres akituma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki dunia huku waliojeruhiwa akiwatakia kupona kwa haraka.

Katibu Mkuu amesema vurugu na hofu havitaleta suluhisho kwa mgogoro kati ya Israeli na Palestina na badala yake vitachagiza kasi ya mzozo huo.

Ametaka wale wote waliohusika na kitendo hicho wafikishwe mbele ya sheria.

Amesema kitendo hicho hakipaswi kuruhusiwa kuuzia nia ya kuongeza upya jitihada za mazungumzo