Skip to main content

WFP yaanza kutoa pesa taslim kwa wakimbizi wa ndani, Darfur

WFP yaanza kutoa pesa taslim kwa wakimbizi wa ndani, Darfur

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kwa usaidizi kutoka serikali ya Uingereza, limezindua mpango wa kutoa msaada wa pesa taslim kwa wakimbizi katika kambi ya Otash iliopo Nyala, Darfur ya Kusini, nchini Sudan.

WFP imesema msaada huo wa karibu dola milioni nne na nusu wa kutoa pesa taslim katika kambi hiyo, ni sehemu ya mpango wake wa kuendeleza juhudi za kutoa mbinu mpya zinazoendana na matakwa ya walengwa ili kutokomeza njaa na kuwaepusha utegemezi.

Kwa sasa Uingereza kupitia mfuko wake wa Msaada UK aid, inatoa msaada wa pesa taslim kwa wakimbizi wa ndani takriban 75,000 nchini Sudan.