Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na EU washirikiana kukwamua uhaba wa chakula Yemen

FAO na EU washirikiana kukwamua uhaba wa chakula Yemen

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limepokea Euro milioni 12 kutoka Muungano wa Ulaya, EU ili kukwamua watu watu milioni 14 wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula nchini Yemen. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Fedha hizo pamoja na kutumika kutathmini kiwango cha uhaba wa chakula Yemen, pia zitatoa usaidizi wa kilimo kwa watu zaidi ya 150,000 ili waimarishe uzalishaji wa chakula na kuboresha lishe.

Nchini Yemen kilimo kina nafasi kubwa katika kukabiliana na ukosefu wa chakula hasa kwa wakazi wa vijijini ambako ukosefu wa usalama na misaada ya kibinadamu ni jambo la kawaida.

Kwa mantiki hiyo kupitia fedha hizo, wanufaika wataweza kuanzisha miradi ya ufugaji kuku, ng’ombe, nyuki na pia kupata mbinu mpya za kilimo, ufugaji na usindikaji aw vyakula.

Dominique Bourgeon ni Mkurugenzi wa masuala ya dharura FAO.

(Sauti ya Dominique)

“Kutusaidia kushughulikia suala kubwa Yemen ambalo ni uhaba wa maji, ambapo tutaanzisha vikundi vya watumiaji wa maji na ununuzi wa vifaa vya umwagiliaji na mafunzo ya matumizi bora ya maji.”