Hali ya maisha kwa wakimbizi waSyria walioko Lebanon ni ngumu-UNHCR

Hali ya maisha kwa wakimbizi waSyria walioko Lebanon ni ngumu-UNHCR

Utafiti wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiratibiwa na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini unaonyesha kuwa ukosefu wa chakula na umasikini vinawakabili wakimbizi wa Syria walioko nchini Lebanon.

Utafiti huo wa kila mwaka ulioshirikisha pia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la mpango wa chakula WFP unaonyesha pia kuwa asilimia 71 ya kaya za wakimbizi hao 71 nyingi huishi katika ufukara.

Mkurugenzi wa UNHCR Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Amin Awad amesema wakimbizi hawa wanakabiliana vigumu na wanategemea msaada kutoka jumuiya ya kimataifa. Akiongeza kuwa bila ya kuupata hali yao itakuwa mbaya.

Utafiti huu wa nne wa aina yake na hufanywa kwenye mazingira magumu na matokeo hutumika katika njia mbalimbali ikiwemo kusaidia walengwa wa misaada.  Lebanon inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Syria.