Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres azungumza na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki

Guterres azungumza na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki

Takribani wiki moja baada ya shambulio la kigaidi lililolenga washerehekeaji wa mwaka mpya, katika klabu moja ya usiku nchini Uturuki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekutana na kuzungumza na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mevlüt Çavuºoðlu.

Katibu Mkuu amempa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Uturuki kufuatia athari za shambulio hilo, ikiwamo lile la mjini Izmir.

Viongozi hao wawili wamejadili hali nchini Syria, ambapo Guterres ameshukuru Uturuki kwa kuhifadhi wakimbizi milioni 2.8 wa Syria pamoja na kulishukuru taifa hilo kwa usaidizi wake katika kusitisha mapigano na mchakato wa amani ya Syria..

Kadhalika wamejadili suala la mgogoro wa Cyprus na maandalizi ya mkutano kuhusu nchi hiyo utakaofanyika Geneva Januari 12, huku Katibu Mkuu akizitaka pande kinzani kusaka suluhu ya mgogoro huo.