Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabila ridhia hadharani mkataba wa kisiasa - OHCHR

Kabila ridhia hadharani mkataba wa kisiasa - OHCHR

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC anapaswa kuunga mkono hadharani makubaliano ya kisiasa ambayo yanaweka bayana masuala ya uchaguzi huru na wa haki nchini humo. Grace Kaneyia na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Wito huo umetolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR kufuatia kutiwa saini kwa mkataba huo wa kisiasa tarehe 31 mwezi uliopita huko Kinshasa.

Liz Throssell ambaye ni msemaji wa ofisi hiyo akizungumza na waandishi wa habari amesema.

(Sauti ya Liz)

“Ni muhimu kwa serikali, vyam a vya upinzani, mashirika ya kiraia na wananchi wa DRC kufanya kazi kuhakikisha utekelezaji wa mkataba huo na kuweka mazingira sahihi ya kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi huru, wa haki na halali. Kwa hiyo basi tunamsihi Rais Kabila aidhinishe mkataba huo hadharani.”

Makubaliano hayo ya kisiasa yaliyoratibiwa na jumuiko la maaskofu wa kikatoliki nchini humo yalifikiwa baada ya maandamano yaliyoghubikwa na ghasia nchini humo, maandamano ambayo yalikuwa yanapinga kitendo cha Rais Kabila kupinga kuondoka madarakani baada ya kipindi chake cha uongozi kumalizika tarehe 19 mwezi uliopita.

Takribani watu 94 yaripotiwa waliuawa wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama.