Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bi. Muller ateuliwa naibu mkuu wa OCHA

Bi. Muller ateuliwa naibu mkuu wa OCHA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Ursula Mueller wa Ujerumani kuwa msaidizi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu, OCHA.

Bi. Muller anachukua nafasi ya Kyung-wha Kang ambaye ameteuliwa kuwa mshauri mwandamizi wa Katibu Mkuu kuhusu sera.

Naibu Mkuu huyo wa OCHA ana uzoefu wa miaka 30 kwenye masuala ya kimataifa pamoja na changamoto zinazokabili dunia, bila kusahau uchangishaji kwa ajili ya maendeleo.

Tangu mwaka 2014 amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi tendaji ya benki ya dunia akiwajibika na masuala muhimu ya kimkakati ikiwemo uidhinishaji wa bajeti ya dola bilioni 62 mwaka 2016.

Amehudumu pia katika nyadhifa mbali mbali za serikali ya Ujerumani ikiwemo Naibu Mkurugenzi wa wizara ya mambo ya kigeni na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini mwake.