Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa ya hifadhi kwa wakimbizi wa Somalia haitabinywa

Fursa ya hifadhi kwa wakimbizi wa Somalia haitabinywa

Nchi tano za pembe ya Afrika zinazohifadhi wakimbizi wa Somalia, zimesema zitaendelea kuwapatia hifadhi wakimbizi hao wakati huu ambapo harakati zinaendelea kurejesha amani ya kudumu nchini mwao. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats…

Mohammed Abdi Affey huyu ambaye ni mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa wakimbizi wa Somalia, akiwapatia muhtasari waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi hii leo, ripoti ya ziara yake kwenye nchi zinazohifadhi wakimbizi wa Somalia kwa miaka 25 sasa.

Ametembelea Kenya, Yemen, Uganda, Djibouti, Ethiopia na Somalia akisema lengo ni kushawishi fursa zao za hifadhi zisibinywe, akisema marais wa nchi hizo wamekubali lakini kubwa ni

(Sauti ya Mohammed-1)

“Kuongeza maradufu jitihada za kuleta utulivu Somalia na usaidizi zaidi kwa wenyeji wanaohifadhi wakimbizi kwani hii inapunguza msuguano kati ya wakimbizi na wenyej.”

Alipoulizwa kuhusu wakimbizi wasio wa kisomali kwenye kambi ya Daadab, Bwana Affey amesema..

(Sauti ya Mohammed-2)

“Serikali ya Kenya sasa imeanza kufuta utambulisho wa ukimbizi kwa raia wa Kenya walioingia kambini kwani wote wanatoka jirani na kambi ambako kuna changamoto za maisha. Huu ni mchakato, mchakato ambao unafuatiliwa na serikali ya Somalia, Kenya na UNHCR.”