Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yafundisha vijana stadi za ufundi

MONUSCO yafundisha vijana stadi za ufundi

Kikosi cha Pakistani kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimeanza kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana kama njia mojawapo ya kuimarisha usalama na hatimaye kutokomeza umaskini.

Taarifa ya MONUSCO imesema vijana 41 wakiwemo wasichana wanne kutoka jamii mbali mbali kweney mji wa Uvira, jimbo la Kivu Kusini wanashiriki mafunzo hayo ya ufundi mchundo ikiwemo umeme, umakenika na useremala.

Mkuu wa kikosi hicho Meja Khalil amesema mafunzo hayo yanayotolewa bure yanalenga kuwapatia vijana stadi zitakazowawezesha kujumuika katika jamii na hivyo kukabiliana na umaskini na kuepuka vishawishi vya kutumikishwa kwenye vikundi vilivyojihami.

Mafunzo hayo yanatolewa bure na walinda amani kutoka Pakistani ambapo Meja Khalil amesema yatafanyika kwa wiki nne au zaidi iwapo italazimika kuongeza muda.