Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kobler aonya uwezekano wa migogoro mipya Libya

Kobler aonya uwezekano wa migogoro mipya Libya

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler ameonya juu ya hatari ya kuzuka kwa migogoro mipya kufuatia mwelekeo wa hali ya sasa nchini humo.

Kobler ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL kupitia taarifa yake ameziomba pande zote kujizuia na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo ya amani.

Halikadhalika ametoa wito pande kinzani zisake suluhu za maridhiano kuanzia ngazi ya mashinani hadi taifa na kuepuka kitendo au kauli zozote zinazoweza kuchochea hali mbaya zaidi.

Mwakilishi huyo maalum amesisitiza umuhimu wa jitihada mpya za haraka ili kutatua  masuala ya kisiasa na hivyo kuruhusu utekelezaji kamili wa mkataba wa kisiasa wa Libya huku akiunga mkono harakati zinazoendelea dhidi ya ugaidi nchini humo.