Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha MINUSCA chashambuliwa, wawili wapoteza maisha

Kikosi cha MINUSCA chashambuliwa, wawili wapoteza maisha

Askari wawili walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. MINUSCA, wameuawa baada ya kushambuliwa na kikundi cha watu wasiojulikana na waliojihami kwa silaha . Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Msemaji wa MINUSCA Vladimir Monteiro ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa askari waliouawa katika shambulio hilo la hapo jana wanatoka katika kikosi cha Morroco, ambacho kilikuwa kikitekeleza wajibu wake wa kusindikiza lori kutoka eneo moja hadi jingine.

Amesema walinda amani wengine wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo, mmoja vibaya, na wote wanaopatiwa matibabu.

Bwana Monteiro licha ya kulaani shambulio hilo amesisitiza.

( Sauti Monteiro)

‘‘Jambo muhimu zaidi kwetu ni kusaidia mchakato wa majadiliano yaliyoandaliwa na Rais wa CAR, ili kuvipokonya silaha vikundi hivi, kwa kupitia mpango wa kuwajumuisha yani DDR. Mwezi Disemba mwaka jana vikundi 11 kati ya 14, vilihudhuria mkutano. MINUSCA inatia shime zaidi ili vikundi vyote vihusike katika majadiliano haya ya DDR.’’