Skip to main content

Marekebisho ya katiba Sudan Kusini ni msingi wa maendeleo- UNMISS

Marekebisho ya katiba Sudan Kusini ni msingi wa maendeleo- UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umesema suala la marekebisho ya katiba nchini humo ni jambo linalopaswa kupatiwa kipaumbele mwaka huu wa 2017 ili kufanikisha mchakato wa amani. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Mkurugenzi wa UNMISS anayehusika na masuala ya siasa, Seth Kumi amesema hayo akihojiwa na Radio Miraya ya ujumbe huo akisema kuwa suala hilo ni muhimu ili kujumuisha misingi ya mkataba wa amani kwenye katiba ya muda.

(Sauti ya Seth)

“Bado Tume ya marekebisho ya katiba haijaanza kazi, na pia tungependa kuona kamati ya mapitio ya katiba na pia dola na bunge vifanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza sheria ambazo zitatoa hakikisho la haki za binadamu na fursa za demokrasia. Mnapokinzana kisiasa haimaanishi ni maadui, na sote tuna lengo moja.”

Bwana Seth amesema bila masuala ya kisiasa kupatia jibu, itakuwa vigumu kwa Sudan Kusini kutekeleza mipango ya maendeleo.