Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujitolea kufanyike kwa upendo na si kwa hila- VION

Kujitolea kufanyike kwa upendo na si kwa hila- VION

Mratibu wa kitaifa wa shirika la kujitolea nchini Kenya, VION, Fredrick Sadia amesema kazi ya kujitolea inawezesha mtu kufahamu mahitaji ya watu wengine na pia kuwasaidia kwa upendo ili kuboresha maisha yao.

Bwana Sadia amesema hayo hivi karibuni alipohojiwa na Umoja wa Mataifa huko Mexico Marekani akisema.

(Sauti ya Fred Sadia)

“Kujitolea kunaridhisha kila unapoamka asubuhi na uko tayari kuifanya tena na tena. Halikadhalika kunaleta ushawishi kwa wengine kwani watu wanaona kazi inayofanywa ya kujitolea na wangependa kujiunga ili kwa pamoja wafanye jambo zuri ambalo ni jema kwa wote.”

Bwana Sadia ambaye pia ni katibu wa shirika hilo amesema kujitolea ingawa hatua wanazochukua zinaweza kuonekana ndogo lakini bado zinaleta mabadiliko, huku akiwa na ujumbe kwa wanaotaka kufanya kazi ya kujitolea.

(Sauti ya Sadia)

Fanya kwa upendo, fanya kwa maslahi yaw engine, na iwapo unafanya kwa nia nyingine ya siri, basi wewe si mfanyakazi wa kujitolea, bora utafute kitu kingine ufanye.”