Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu Côte d'Ivoire kuangaziwa

Haki za binadamu Côte d'Ivoire kuangaziwa

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kujenga uwezo wa kidemokrasia na ushirikiano wa kiufundi huko Côte d'Ivoire, Mohammed Ayat ataanza ziara ya Nane nchini humo akiangazia masuala ya haki za binadamu. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu imesema ziara ambayo ni ya tano nchini humo itamwezesha Bwana Ayat kuangazia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa taasisi za kidemokrasia, kuimarisha utawala wa sheria na haki za msingi za binadamu.

Mathalani ataangazia hatua zinazofanyika kuwezesha nchi hiyo kusimamia na kuzingatia haki za binadamu kupitia Tume ya Taifa ya haki za binadamu kwa kutambua kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo utahitimisha shughuli zake tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo, mtaalamu huru huyo atakutana na pande mbali mbali ikiwemo viongozi wa serikali ya Côte d'Ivoire, wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika.

Ripoti ya ziara yake itawasilishwa mbele ya Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, mwezi Juni mwaka huu.