UM walaani mauaji ya Waziri Burundi

UM walaani mauaji ya Waziri Burundi

Umoja wa Mataifa umesema mauaji ya Waziri wa Maji na Mazingira nchini Burundi, Emmanuel Niyonkuru, ni jambo la huzuni na ni kiashiria kingine ya kwamba pande kinzani nchini humo zikae pamoja na kusaka suluhu ya kudumu ya mzozo wa kisiasa nchini humo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini New York, Marekani na kuelezea masikitiko ya chombo hicho kufuatia mauaji hayo ya tarehe mosi mwezi huu.

Amesema Umoja wa Mataifa unasihi kuwepo kwa utulivu na ukisihi serikali ifanye uchunguzi wa haraka na halali dhidi ya mauaji hayo na zaidi ya yote.

(Sauti ya Dujarric)

“Umoja wa Mataifa uko tayari kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na wadau ili kusaidia uwezeshaji wa mashauriano yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

Umoja wa Mataifa umetuma salamu rambirambi kwa serikali ya Burundi, wananchi wake na familia.