Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa ni msingi wa suluhu za changamoto za dunia hivi sasa- Guterres

Umoja wa Mataifa ni msingi wa suluhu za changamoto za dunia hivi sasa- Guterres

Katibu Mkuu wa tisa wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amewasili katika makao makuu ya umoja huo ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi katika nafasi hiyo ya juu kwenye chombo hicho. Joseph Msami ameshuhudia kwa kuwasili kwake na kutuandalia taarifa ifuatayo.

(TAARIFA YA MSAMI)

Nats!

Katibu Mkuu ndio anawasili hivi sasa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mtaa wa kwanza, Barbara ya 42 mjini New York.

Wafanyakazi wanamlaki, anawasilimia, na kisha anaelekea jukwaani kuzungumza na wafanyakazi. Awali Katibu Mkuu ameweka shahada la maua kwa heshima ya wafanyakazi waliopoteza maisha. Jukwaani analakiwa na Naibu Katibu Mkuu wake Amina J Mohamed na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Akiongea na wafanyakazi Katibu Mkuu amegusia ushirikiano wa kimataifa akisema hakuna nchi moja pekee inayoweza kutatua changamoto za sasa hivyo...

Guterres-1

“Huu ni wakati ambao tunapaswa kusisitizia thamani ya ushirikiano wa kimataifa, wakati wa kutambua kuwa suluhu za kimataifa zinaweza kupatikana kimataifa na Umoja wa Mataifa ndio msingi wa kimataifa.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisalimiana na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Mark Garten)
Kuhusu mafanikio ya Umoja wa Mataifa amesema...

Guterres-2-

“Mambo yote haya tunapaswa kujivunia, lakini pia tunapaswa kutambua changamoto zetu, kushindwa kwetu na mazingira ambamo kwayo tumeshindwa kufanikisha kwa ajili ya watu tunaowahudumia.”

Kisha Katibu Mkuu Guterres ametoa mapendekezio yake namna ya kuboresha chombo hicho.

Guterres-3

“Tunapaswa kuhakikisha kuwa tuna uwezo wa kurekebisha mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa kama nchi wanachama walivyotaka na pia tujaribu kuondokana na ukiritimba unaofanya maisha yetu yawe magumu.”