Ukata wafungisha vituo vya afya nchini Sudan - WHO

3 Januari 2017

Ukata huko nchini Sudan umesababisha kufungwa kwa vituo 11 vya afya na kuacha vingine 49 vikiwa hatarini kufungwa. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Shirika la afya duniani, WHO linasema hatua hiyo inaathiri karibu watu milioni moja wakiwemo wanawake 323 000 wenye umri wa kubeba ujauzito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Idadi hiyo inaweza kuwa kubwa kutokana na wimbi la wakimbizi nchini Sudan, ikielezwa kuwa kufungwa kwa vituo vya afya kutaongeza hatari iliyoko sasa ya mlipuko wa magonjwa kutokana na upatikanaji mdogo wa huduma za afya ya msingi.

Mwakilishi wa WHO nchini Sudan Dkt Naeema Al-Gasseer amesema japokuwa serikali kupitia Wizara ya Afya inajaribu kusaka uwepo wa huduma, bado fedha zinahitajika kuendelea kusaidia kliniki za mama na mtoto kwenye maeneo ya vijijini ili kutoa huduma wakati wa kipindi hiki cha mpito.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter