Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rununu kuinua elimu Tanzania: UNESCO

Rununu kuinua elimu Tanzania: UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO nchini Tanzania, linaendesha mpango wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za sekondari nchini humo kutumia teknolojia ya rununu kunufaika zaidi kielimu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya UNESCO, Dk. Moshi Kimizi ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa mpango huo unaotekelezwa Pemba Tanzania Zanzibar, utawasaidia kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na kuitumia kujinufaisha kielimu.

(Sauti Kimizi)

Dk kimizi amesema mpango huo umeanza kwa mafunzo maalum kwa walimu wa shule ya sekondari ambapo pia utungaji wa mitihani wezeshi umejadiliwa.

(Sauti Kimizi)