Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji milioni 2 Ethiopia wahitaji misaada ya dharura- OCHA

Wafugaji milioni 2 Ethiopia wahitaji misaada ya dharura- OCHA

Nchini Ethiopia wafugaji wapatao milioni Mbili wanahitaji msaada wa dharura wa chakula kutokana na uhaba mkubwa wa maji unaoendelea kukabili maeneo ya Oromia, Somali na Afar nchini humo.

Chapisho la ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA limesema hali hiyo inatokana na ukame uliochagizwa zaidi na hali ya El Nino nchini humo pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi.

OCHA imesema uhaba huo umefanya idadi ya waethiopia waliokwamishwa vipato vyao mwishoni mwa mwaka jana kufikia milioni 9.7 na hivyo ofisi hiyo inahitaji fedha za dharura kukidhi mahitaji hususan ya kudhibiti magonjwa kama vile Kipindupindu.

Hata hivyo ofisi hiyo imesema takwimu rasmi za watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu Ethiopia itatolewa rasmi mwezi huu.